Saturday, June 11, 2011

WABONGO NA USINGIZI WAO MTAMU!

JE, RISASI KWA MSOUTH AFRICA BANDIA "DANIEL ROBINSON" HUKO SOMALIA ZILIESABABISHA HII.....


Fazul-dead.jpg


.... KWA HUYO MSAUZI-BANDIA (ROBINSON).....


Fazul Abdullah Mohammed (FBI)


....YAWAHAKIKISHIA WABONGO (WAKAZI WA DAR ES-SALAAM) USINGIZI MTAMU NA MATUMAINI HAPATATOKEA TENA HAYA.......?


tanzaniaembassybombing.jpg




Picha hizi, kwa kufuatiliana, tumezipata kwa "The Long War Journal"  , "BBC News Africa"  na mtandao wake Debbie Schlussel






Siku tatu baada ya kuuliwa kwake Fazul Mohammed (kiongozi wa Al Qaeda Afrika Mashariki) aliepatikana na paspoti bandia ya Afrika Kusini (kama inavyoripotiwa) Labda ni malizie kwa kuomba msaada wa majibu yenu wasomaji:

KWANINI MAADUI WA HUKO MBALI WANAPENDA KUPIGANA VITA VYAO HAPA KWETU AFRIKA?




JE, NI UKWELI KWAMBA KWA WATU WANJE NA BARA LETU MWAFRIKA ANAONEKANA KAMA TAMBALA MBOVU LA KUKANYAGWA UPENDAVYO TU WALA WAAFRIKA SIO NAO BINADAMU NA VIUMBE VYA MUNGU?  




KWA WALIEMLENGA MWAMERIKA HUKO DAR ES-SALAAM MIAKA ILIEPITA NA KUBOMOA UBALOZI WAO KAMA PICHA INAVYOONYESHA, KWANINI HAWAKUHAKIKISHA MAISHA YA MWAFRIKA ASIEKUWA NA HATIA YATASALIMIKA KABLA YA KUSHAMBULIA UBALOZI HUO?




TUFANYE NINI SISI WAAFRIKA ILI MAKABILA MENGINE, MZUNGU KWA MWAARABU (NJE YA BARA LETU) YATUTAMBUE NASI KAMA WATU SAWASAWA NAO?

2 comments: