Monday, September 5, 2011

NIMEKIONA CHA MTEMAKUNI HAPO JANA!



Tuache utani sasa: Je, kweli hii sio uonevu?


Mtoto mimi bado mchanga kabisa; wala sijamaliza hata huo mwaka mmoja nalo libaba jana linanileta katika sehemu kama hii!

Makubwa! Na viitoto vimejaa hapa kibao; wala mimi simtoto wakipekee tena wala sio maalum!  Maalum kwa nani...? SIONI BABA SIONI WALA MAMA!


Nimeamua kuwakomoa tu hao wawili: silii wanaponiacha asubuhi saa moja na nusu katika shule hii, wala siwapokei kwa shamrashamra wanapokuja kunichukua jioni saa tisa! Wao wanajiona kama nani kwangu...? ...Mungu mwenyezi mwenyewe...?!


Siku moja watazeeka kama Robert Mugabe (Baba huyo) na vilevile kama Malkia Elizabeth (Mama huyo mwenye kukubaliana na Baba kama kipofu vile tena chenye kusahau maumivu ya kumzaa mtoto)....


....Na wakishazeeka mimi nitakuwa basi ndio mwenye nguvu na mwenye uamuzi wakipekee... UNILATERAL DECISIONS... kama walivyonifanya jana Mtoto mchanga mimi kunipeleka katika watoto wengi nisiewafahamu nje ya makamasi yao ya hovyo tu! (nilipoondoka,  litoto limoja limethubutu hata kuniambia: "Tamara, urudi kesho hapahapa, la sivyo tutakuja kukupiga!")


Basi uzeeni wao wazazi wangu nabadili hata majina yao: Goodman siGoodman tena, na atakuwa Badman.  Naye Hlob'sile (mama mwenye jina la "Mapambo" kwa Kiswahili kutoka Siswati, nitampachika jina la "Mabaya")

Mimi sifanyiwi hivyo kupelekwa huku na huko tena hovyo bila kufanyiwa mahojiano nataka au sitaki! Mimi Matanje Wa Mphuno-nga-Ndunyungu sifanyiwi kama gari mbovu kabisa!


WATAKUJA KUNIFAHAMU TU!!!!

10 comments:

  1. Jamani mwanangu wamekupeleka shule? pole sana mama lakini ndiyo mwanzo da'Tamara, huko utakutana na wababe na wapole mama, kaza buti kama vipi njoo huku, duh lakini hata mimi nitakupeleka hukohuko mwanakwetu.Mungu akulinde na kukuza vyema.

    ReplyDelete
  2. Asante, Shangazi kwa kuwanusurisha hao wazazi wangu. Kumbe ndivyo dunia ya watoto inavyokwenda kotekote!

    ReplyDelete
  3. Si uongo hata kidogo, watoto mbona wanakionaga cha moto?

    ReplyDelete
  4. @Mija

    Mama Mdogo alinifunza kitu kimoja kuhusu watoto hata wa miezi michache au wiki tu tangu kuzaliwa: ONGEA NAYE NA UMUELEZE KILA HATUA UNAYOCHUKUA NAYE.

    ReplyDelete
  5. Ni kweli kabisa kuongea na mtoto pamoja na kumshirikisha katika maamuzi hujenga sana tabia ya kujiamini, kwa njia hiyo mtoto huondoa uoga na kuwa mdadisi popote anapokwenda..

    ReplyDelete
  6. Masikini,atazoea tuu mwanzo huwa mgumu.

    ReplyDelete
  7. nitamleta wangu huko ili apate orientation kutoka kwa huy mkubwa wake

    ReplyDelete
  8. @Mija
    Asante sana kwa kunitobolea siri ya mfadhaiko wangu mara hadi mara! Lile limama lilikuwa halinijumuishi katika maamuzi yalo ndio maana...!(LOL!)

    @Edna
    Ameshazowea tayari, asante kwako, Wangu Edna!


    @Kamala
    Tena watawezana vizuri. Tamara anawapenda watoto wengine sana. Lakini kuja hapa Binti Kamala lazima awe amevaa mawani tena baada ya kujaza kabisa tumbo lake na mboga, maana yake...


    Kwanza, Tamara kumtambua rafiki hata mimi mzazi wake kutambulika, lazima aingize kidole machoni yako kwanza na huko shuleni ya vidudu wamekerwa na hilo... na natarajia wamfukuze wakati wowote ule! (LOL)

    Pili Tamara anakula ugali hapo tu ukiwa "mkavu": weka mboga au nyama pamoja na ugali huo ndipo hatakula kabisa! Nina hisi Ni hiyo burudhani tu katika ulaji wake inayomponyesha asifukuzwe shule kwa kutoboa-toboa macho ya waliolala!

    ReplyDelete
  9. Najiuliza tu sijui anafikiria nini katika hiyo Picha!

    Nadhani ukidadisi labda haelewi kabisa kwanini anapelekwa hapo!

    ReplyDelete
  10. Kabisa! (Vilevile nimesoma kitabu kimoja kinachoelezea kuhusu Synesthesia, yaani kwamba kwa watoto, kawaida wanaweza wakasikia kitu kwao kiwe kama radha mdomoni, wakaona kitu au rangi fulani ikawa kama wimbo mzuri au mbaya; wakanusa kitu halafu kuhisi anakigusa vile, hata kuonja kitu na kuona kama radha yake ni rangi fulani NA MAMBO YOTE KAMA HAYO... na hiyo Synesthesia inaharakisha kwa watoto kusoma vitu haraka kuliko watu wazima...mfano: lugha ya kigeni!)

    ReplyDelete