Showing posts with label Tamara Sibusisiwe Phiri first day in crèche shule ya vidudu. Show all posts
Showing posts with label Tamara Sibusisiwe Phiri first day in crèche shule ya vidudu. Show all posts

Monday, September 5, 2011

NIMEKIONA CHA MTEMAKUNI HAPO JANA!



Tuache utani sasa: Je, kweli hii sio uonevu?


Mtoto mimi bado mchanga kabisa; wala sijamaliza hata huo mwaka mmoja nalo libaba jana linanileta katika sehemu kama hii!

Makubwa! Na viitoto vimejaa hapa kibao; wala mimi simtoto wakipekee tena wala sio maalum!  Maalum kwa nani...? SIONI BABA SIONI WALA MAMA!


Nimeamua kuwakomoa tu hao wawili: silii wanaponiacha asubuhi saa moja na nusu katika shule hii, wala siwapokei kwa shamrashamra wanapokuja kunichukua jioni saa tisa! Wao wanajiona kama nani kwangu...? ...Mungu mwenyezi mwenyewe...?!


Siku moja watazeeka kama Robert Mugabe (Baba huyo) na vilevile kama Malkia Elizabeth (Mama huyo mwenye kukubaliana na Baba kama kipofu vile tena chenye kusahau maumivu ya kumzaa mtoto)....


....Na wakishazeeka mimi nitakuwa basi ndio mwenye nguvu na mwenye uamuzi wakipekee... UNILATERAL DECISIONS... kama walivyonifanya jana Mtoto mchanga mimi kunipeleka katika watoto wengi nisiewafahamu nje ya makamasi yao ya hovyo tu! (nilipoondoka,  litoto limoja limethubutu hata kuniambia: "Tamara, urudi kesho hapahapa, la sivyo tutakuja kukupiga!")


Basi uzeeni wao wazazi wangu nabadili hata majina yao: Goodman siGoodman tena, na atakuwa Badman.  Naye Hlob'sile (mama mwenye jina la "Mapambo" kwa Kiswahili kutoka Siswati, nitampachika jina la "Mabaya")

Mimi sifanyiwi hivyo kupelekwa huku na huko tena hovyo bila kufanyiwa mahojiano nataka au sitaki! Mimi Matanje Wa Mphuno-nga-Ndunyungu sifanyiwi kama gari mbovu kabisa!


WATAKUJA KUNIFAHAMU TU!!!!