Tuesday, June 14, 2011

ASEMA HAELEWI KWANINI MWIZI UMSAMEHE NA PIA UMWACHIE NA KILE ALIEKIIBA

IOL pic jun15 julius malema land rights
JULIUS SELLO MALEMA, AGED 30 (CREDIT THIS PICTURE TO THIS LINK)





Kiongozi wa Vijana Afrika Kusini, Julius Sello Malema (nusu kusema Julius Nyerere)... kwani hawa akinaJulius wakweje kwa ukereketwa, Jamaani.....?




... Amesema leo haelewi kabisa yeye kwanini kwanza Wazungu walisamehewa kwa uhalifu na ukatili wao wa mfumo wa Apartheid Afrika Kusini kabla ya mwaka1994, wakiwa wanasemehewa na huyo raisi wetu maarufu wakwanza....




...Kijana anasema hata kama anawuelewa huo msamaha, anashindwa kabisa kuelewa kwanini baada ya kusamehewa kwao [lakini maeneo ya nchi waliyoiba kwa Waswahili hapa Bondeni tangu mwaka 1652 yameaachiwa kwao hivyohivyo na sasa Waswahili wanatakiwa eti wanunue ili waweze kufanya kilimo na mambo kama hayo].




Yeye kama kiongozi waVijana wa chama tawala, anapendekeza Waafrika wapewe bure; yaani Mzungu mwenye ardhi popote pale nchini inaotakiwa na Mswahili, anyang'anywe tu bila malipo yoyote kwani babu yake Mzungu naye aliwanyang'anya Waafrika.  Kiongozi wa vijana huyo anafikiri kwa maoni yake, Mzungu huyo mwenye kunyang'anywa ardhi hiyo ashukuru tu amesamehewa na hakupelekwa mahakamani.




Maoni ya huyo kiongozi siyo ya kigeni, kwani Waswahili wakereketwa kotekote duniani wanalaani sana jinsi uhuru wa Bondeni hapa ulivyopatikana, wakiwa na imani kwamba labda kiongozi huyo wakwanza alitumika kama kibaraka cha wakoloni mambo leo.  Ebu, angalia hii video yake msomi Doctor Khalid Muhammad naye anayeulliza [kama Wayahudi waliewahi kukandamizwa kama Waswahili wa Afrika Kusini, baada ya uhuru wao waliwapeleka wakandamizaji kortini za Nuremberg, kwanini Waswahili Afrika Kusini hawakupeleka Wazungu kortini za 'Johannesberg'?




Mnasemaje, Wadau? Afrika Kusini inaelekea wapi hivi? Kiongozi huyo anamaana yoyote? Au anazungumza tu ili apate kuchaguliwa tena awamo ya pili?




(Jina lake kiongozi huyo la Kiswahili, "Sello":taama kama umeona, tena kwa mshangao, kitu kinachoitwa "SIL" na kwa hiyo unapaaza sauti  kwa mshangao: "SIL- LO!", wala usitamke SELO au SILO!)  Hilo jina linamaana "kilio" kwa lugha za KiSotho (Pedi, Tswana, South Sotho).  Historia yake kidogo: amezaliwa Jumanne, Tarehe 3 March 1981, na sasa anamika 30.28337, akiwa na mzazi mmoja tu kwani baba mtu alimtelekeza baada ya kumpa mimba mama yake.  Baada ya kifo cha mama yake aliekuwa anawafanyia Wazungu kazi za uhauzigeli, na baada yake kuchaguliwa kiongozi wa vijana katika chama chake, libaba lilijitokeza ghafla eti kupata michuzi, au sio?  Inasemekana kijana Sello alimshukuru huyo baba kwa kujitmbulisha kwake lakini alimuomba arejee hukohuko alikotokea kwani angekuja labda kabla ya kifo cha mama yake, au kabla ya yeye kupata mateso makubwa alipohudhuria shule kwa msaada wa mama maskini peke yake, angemkubali kwamba kweli ni baba!)


.....MADOGO YANANAFUU!

No comments:

Post a Comment