Sunday, January 1, 2012

WAKATI HASWA NDIO HUU..HEPI 2012!

HERI YA MWAKA MPYA-2012!  Wengine tumejifunza mabaya.  Yaani watoto wengine wanasherehekea mwaka mpya nasi huku tunafanya kazi kama kawaida!

Vibaya namna hiyo! Nami mwenye mtindo huo  nimekuja kujikosoa sasa. Najirudi kabisa!


Lakini Bwana wakati mwingine hua siamini nimepata chakula kama nakiona kwenye sahani tu.  Lazima kwanza angalau tonge moja la ugali likae kinywani ndipo nitaamini chakula hicho nimepewa mimi kabisa.

Ni kwa hiyo sababu tu ya msingi nilikawia kidogo kuwatakieni wote wasomaji wa blogu yangu mpya Heri ya mwaka mpya 2012!  Ni kama siamini blogu hii imeanza mwaka-jana tu lakini imeshapata wasomaji idadi kama wewe hapo Msomaji mheshimiwa mojawapo!


Huyo mwimbaji Beau Williams amenifanya vilevile nimkumbuke Mke Wangu wa pili, Bibi Hlob'sile Happy Tsabedze-Phiri ambae kwa wakati zaidi ya wiki sasa amekwenda kutembelea ndugu zake Soweto na kuniacha na upweke hapa Pretoria.

Anastahili mapumziko mbali na simba kwa wakati mwingine, kwani mwanamke amepata mwaka 2011 mgumu sana.  Pamoja na malezi ya mtoto mdogo, ameshuhudia nikishambuliwa huku na huko na maadui zangu na kazi ya kubembeleza ilikuwa ya kwake peke yake ninapolia na kutoa hasira.

Ameniona pia nikiwa na gadhabu zangu tu za kiPhiri, maana yake unaambiwa maana ya "Phiri" ni "Moto" au "Mlima wa Moto".

Ameniona na umaskini. Hela hazitoshi kwa kwa chakula au matumizi mengine ndani ya nyumba.

Ameniona pia na magonjwa yangu.  Ameniona na udhaifu wote wangu, lakini yote kayavumilia.

Haelewi Kiswahili lakini kama hivi naandikia roho yake tu... kwani roho ya binadamu huelewa kila lugha na husikia umbali wowote ule kama pale alipo sasa mke wangue.  Na namuambia

"Nakupenda sana, Mama-mtoto! Heri ya Mwaka 2012! Sijui kama tutapona mwaka huu na maadui tele, lakini mbona Mungu ametuahidi mazuri tu tukimuamini yeye tu!"



4 comments:

  1. mkuu kwa niaba ya wanablogu wa kiswahili (ukiwamo na wewe) ninakuvulia kofia. ubaki wewe na familia yako na wakati mzuri. mwaka 2012 uwe wa mafanikio makubwa

    john mwaipopo
    mbeya tanzania

    ReplyDelete
  2. Furaha yangu, Shemeji Mwaipopo ni kwamba wewe ni mzima. Afrika Kusini peke yake, nimehuzunika kusoma leo asubuhi, tumepoteza maisha ya wato 1000 barabarani kutokana na shamrashamra za sikukuu hizi za Desemba!

    Lakini Shemeji wewe umejichunga kwa ajili ya wale wanaokupenda na kukutegemea. Namshukuru Mungu kwa hilo.


    Kuhusu kofia unaovua, sijui ulipata wapi. Kama nimekupa mimi, leo nakufichulia siri nami nimepewa na wanablogu wanaTanzania walienilea hapa mtandaoni bila kudharau Kiswahili changu!

    ReplyDelete
  3. ..Tena nafichua siri zaidi ni mimi ndo niliyeitoa kofia hiyo na kama bado ningalikuwa nayo hata mimi naungana na kaka Mwaipopo kwamba ningekuvulia kofia hiyo.

    Jamani heri ya mwaka mpya wote huko..
    Mungu akubariki sana mwaka huu kaka.

    ReplyDelete
  4. Asante, Da'Mija! Ubarikiwe, Mtoto wa nyumbani!

    ReplyDelete