Monday, September 2, 2013

IN THE KISWAHILI LANGUAGE: KUTAMBIKA TAMBIKO

1.       Nimekwishajifunza tabia labda mbaya sijui au nzuri ya kutumia maneno kabla ya kuthibitisha uwerevu wangu juu yake.

2.       Kwa mfano: nini  “kutambika”?

3.       Kichwa chake cha Kiswahili-uchwara kimeniambia ni ile namna Mswahili (yaani “African”) anavyojizatiti kuungana au kupata maongezi au hata mawasiliano na Muumba wake kwa kuwapitia mababu na mabibi waliotangulia…..

4.       Hakika nitarekebisha makosa katika posta/post hii kama hapo baadaye najikuta sikuelewa kabisa maana ya KUTAMBIKA TAMBIKO.  Lakini nimeandika hivyohivyo kwasababu nimejifunza kitu kimoja maishani: ukitaka kuelekewa unamaana gani ANDIKA TU KAMA ROHO INAVYOKUTUMA NA REKEBISHA VINGINE HAPO BAADAYE LA SIVYO UTAITSHIA HUTAANDIKA LOLOTE KWA OGA WAKUKOSOLEWA NA MABINGWA BILA MAPROFESA YA LUGHA AU UJUZI NA TAALUMA FULANI AMBAOWEWE KAMA MWANDISHI HUNAYO.  Kwa hiyo: Potelea mbali ukiwa mwandishi mwenye kutaka uhakika juu ya hisia zako!

5.       Turudie basi katika namna ya kuhusiana na Mungu wangu au wako.

6.       Kila dini (na dini ni nyingi hapa Afrika zinakaribia kunichefua mimi binafsi kwani uwingi wake siwuelewi ikiwa Mungu ni mmoja)…lakini kila dini itakwambia jinsi gani ya kujijumiisha na Muumba.  Tatizo ni kwamba kila dini hiyo imeandikwa aidha na Wazingu au Waarabu au watu wa Asia NA WANAMWAMBIA MWAAFRIKA HUYOHUYO MMOJA.

7.       Mimi binafsi sikatai dini yoyote; ila nimejifunza kwamba dini yoyote ile haina maandishi yoyote yenye kukana au kupindua mila na desturi za Kiswahili au Uafrika na jinsi sisi Waafriak an Wakongwe wa Ubinadamu Wopte tulivyokuwa tunawasiliana na Mungu hata kabla ya kuzaliwa kwa Kristu, Buddha au Muhammad.  Na kwahiyo l eo ningependa kujumuika nawe kama msomaji wa blogu yangu jinsi nilivyoelezwa Mswahili (African) wakwanza (hata kabla ya kuzaliwa kwa Mzungu, Mwarabu, au Mchina) alivyokuwa anawasiliana na Mungu wake.

8.       Nitakachokieleza siyo siri yangu wala maandishi matakatifu, bali ni kile nilichoelezwa na wazee Afrika Kusini hapa; na naomba mwenye ujuzi zaidi yangu aongeze kwa maoni yake udhaifu au nyongeza vikiwa vinafaa katika maandishi yangu.  Kwa yote lakini mimi ni mwenye imani ya kwamba Mswahili (African) ameshindwa kuwa mtu katika watu wa dunia kutokana na usiri wake katika mambo yenye kumnufaisha yeye kama dini yake ya kiasili.  Mswahili pia anaaibu sana kujitangaza na kujitembeza, ikiwa ukweli ni kwamba kama lipo taifa lenye sababu la kujigamba kwa chochote kkile, HAMNA LINALOMPITA AU KUMSHINDA MSWAHILI, KWANI SISI WASWAHILI NI BABU AU BINI ZA BINADAMU WOTE DUNIANI.



9.       Kifupi sisemi acha uKrestu au uIslam wako; bali nasema, bali nasema: kusudi bara letu Afrika liende mbele, tafakari vile jinsi Waswahili (Africans) wengi wanavyoendesha maisha yao ya kiroho (spiritual lives). Kwahiyo nakupa katika maandishi ya fuatavyo jinsi nilivyo elimishwa mwaka huu 2013 namna ya kupata mafanikio maishani yako, au kushinda mitihani yote.

10.   Kwanza lazima ujuwe nani ukoo wa baba yako mzazi au pamoja na baba yako mlezi.   Hivyohivyo kwa upande wa akinamama.
11.   Jaribu kujifunza kuhusu mambo hayo kwa kuuliza vitu kama kabila lako na historia kifupi ya na kirefu ya familia yako mazuri na mabaya.
12.   Tafakari au elewa wale watu wa zamani wenye ukoo wako walikuwa wanakula chakula gani… pata ukweli hasaa juu ya huyo babu au bibi unaependa kumsihi akusaidie katika matatizo yako

13.   Ukishapata walikuwa wanakula chakula gani, tafuta unga kidogo sana ili kuwapa WALE.

14.   Labda pia walikuwa wanywaji… sasa pombe gani ilikuwa…FANYA UTAFITI KWA KUWAULIZA WAZEE! (mfano baba yangu mzazi alikuwa mnywaji wa Bols Brandy, na Richelieu na kama namwaza yeye ataweza kuliko wengine kunielewa sioni sababu yakutonunua  kiwango kidogo cha BRANDY yake kumfurahisha)

15.   Kingini cha kwelewa ni kwamba JE WALIVUTA NINI? Afrika Kusini tunaimani kwamba wote wazee wetu wa kale hawakuvuta chochote bali walikuwa watumiaji wa ugoro…. Hapo ni  kazi kwako mwenyewe….

16.   Kwa hiyo ugoro kidogo karibu utakamilisha labda maandalizi ya maombi yako kwa Mungu na kwa wale waliekuwa karibu naMungu wakiwa ndugu zako.

17.   Cha mwisho kabisa labda ni maji: binadamu yeyote aliyewahi kuishi duniani hakuweza BILA MAJI, na kwa hiyo KWANINI UWANYIME MAJI WALE WALIEZOWEA MAJI.

18.   Baada ya kuandaa chote utakayewapa hao Wazee wa kale, kunavipengele kadha wa kadhaa lazima uelewe kabla ya kuwapa wajiburudhishe kwa wakati watakopofikiria jinsi ya kukusaidia katika matatizo yako (SI UNAKUMBUKA YOTE HAYA NI JINSI YA KUJITOA KATIKA MATATIZO FULANI…KESI ZISIYO KUWA NA MWISHO…KUKOSA MPENZI…KUSHINDWA BIASHARA… AU HATA KUSHINDWA KURA KWA WANASIASA…??)

19.   Kama unaishi nyumbani kwa mzazi wako sawa kabisa kwani yote utafanya kama kawaida.  Lakini kama umepanga unanisoma blogu yangu uko hotelini pahala  Johannesburg, Dar es-Salaam, Kenya au hata Tokyo LAZIMA UTOKE KWANZA WENDE PORINI. Ndipo huko utakapowataja wote mababu na mabibi zangu HALAFU KUWAMBIA “KWA SASA HIVI JAMAANI NIKO HAPA NEW YORK, LONDON,AU JOHANNESBURG NIMEPANGA HOTELINI NA NAOMBA MUNIFWATE NIKAWAONYESHENI NINAPO ISHI”

20.   Hapo ulipo ndipo utakapowapea vyakula na vinywaji vyao pia na ugoro au uvutaji wao kama walivuta hiyo bangi, tumbako au chochote kila kutokana na utafiti wakowa ukoo wa zamani. (WENGINE LAKINI HAWAONI KOSA LA KUWAPIA VYAYO HUKOHUKO MISITUNI KAMA WEWE HAUPO NYUMBANI)

21.   Sasa Bibi wa miaka 70 aliyenifunza mwaka huu yote haya alijumuuisha hata mambo ya kutapika name kama mwanafunzi wake nifuata na kufanya inavyostahili kwani alisema ni muhimu ili usiwe na nuksi (nilikuwa naanda kwenda kortini). Binafsi lakini nafikiri mambo ya kujifanya utapike ni ujinga mtupu,  lakini labda mmoja wa wasomaji ataniona kosa kama sielezi namna yake, nayo ni hii:
22.   Robo kikombe ya ‘diwani’ (kama ndio neno sahihi la ‘VINEGAR’) na robo ya kijiko chumvi katika maji vuguvugu kitu kama lita mbili…kunywa asubuhi  AU kabla ya kuongea na Wazee wako au bada…na ingiza au mkono au chocho chenye kusabisha matapiko ya maji hayo. Hapo ndipo umejifanya ‘msafi’ kwa watu wadunia utakavyokabiliana nayo kwa siku hiyo.

23.   Ningependa kumalizia hapa kwa leo,bila kusau maelezo ya fwatao. Posti hii nimefanya kutokana na kwamba sisi WaSwahili ni wasiri sana kuhusu mila na desturi zetu name nafikiri huo ndio ujinga wa kupindukia kwani atajuwaje mtoto aliyekuwa Chuo Kikuu kuhusu mambo yetu kama hatuandiki?  Vilevile usiri wetu huo pia umesababisha matapeli wengi sana kutuibia hela zetu huku wakidai wanatuunganisha na Wazee wetu.

24.   UKWELI NI KWAMBA HUITAJI MGANGA YOYOTE ILI KUTATUA MATATIZO YAKO NA MUNGU AU WAZEEWALIEKUFA! UNAHITAJI TU KUWAELEWAWAO WALIKUWA AKINA-NANI NA WALIPENDELEA VYAKULA GANI NA “WAPE BASI VIDONGE VYAO ILI NAO WAKUPE SULUHISHO KATIKA TATIZO LAKO”


25.   P.S.  Hakikisha kwamba unapoongea nao hao wakubwa MASHARIKI INAKAA KUSHOTO KWAKO!!! (yaani unaangalia kusini mwa ardhi alipoanzia maisha yake Binadamu yote duniani)

Tambiko ni tambiko hata akiwa anamtambika Yesu, Muhammad, Buddha au Babu au Bibi yake Mungu hata ubaguzi juu ya  kumpa majibu kutokana na maombi yake pia na ukweli na uaminifu wa roho yake

No comments:

Post a Comment