Showing posts with label "HERI YA MWAKA MPYA 2012". Show all posts
Showing posts with label "HERI YA MWAKA MPYA 2012". Show all posts

Sunday, January 1, 2012

WAKATI HASWA NDIO HUU..HEPI 2012!

HERI YA MWAKA MPYA-2012!  Wengine tumejifunza mabaya.  Yaani watoto wengine wanasherehekea mwaka mpya nasi huku tunafanya kazi kama kawaida!

Vibaya namna hiyo! Nami mwenye mtindo huo  nimekuja kujikosoa sasa. Najirudi kabisa!


Lakini Bwana wakati mwingine hua siamini nimepata chakula kama nakiona kwenye sahani tu.  Lazima kwanza angalau tonge moja la ugali likae kinywani ndipo nitaamini chakula hicho nimepewa mimi kabisa.

Ni kwa hiyo sababu tu ya msingi nilikawia kidogo kuwatakieni wote wasomaji wa blogu yangu mpya Heri ya mwaka mpya 2012!  Ni kama siamini blogu hii imeanza mwaka-jana tu lakini imeshapata wasomaji idadi kama wewe hapo Msomaji mheshimiwa mojawapo!


Huyo mwimbaji Beau Williams amenifanya vilevile nimkumbuke Mke Wangu wa pili, Bibi Hlob'sile Happy Tsabedze-Phiri ambae kwa wakati zaidi ya wiki sasa amekwenda kutembelea ndugu zake Soweto na kuniacha na upweke hapa Pretoria.

Anastahili mapumziko mbali na simba kwa wakati mwingine, kwani mwanamke amepata mwaka 2011 mgumu sana.  Pamoja na malezi ya mtoto mdogo, ameshuhudia nikishambuliwa huku na huko na maadui zangu na kazi ya kubembeleza ilikuwa ya kwake peke yake ninapolia na kutoa hasira.

Ameniona pia nikiwa na gadhabu zangu tu za kiPhiri, maana yake unaambiwa maana ya "Phiri" ni "Moto" au "Mlima wa Moto".

Ameniona na umaskini. Hela hazitoshi kwa kwa chakula au matumizi mengine ndani ya nyumba.

Ameniona pia na magonjwa yangu.  Ameniona na udhaifu wote wangu, lakini yote kayavumilia.

Haelewi Kiswahili lakini kama hivi naandikia roho yake tu... kwani roho ya binadamu huelewa kila lugha na husikia umbali wowote ule kama pale alipo sasa mke wangue.  Na namuambia

"Nakupenda sana, Mama-mtoto! Heri ya Mwaka 2012! Sijui kama tutapona mwaka huu na maadui tele, lakini mbona Mungu ametuahidi mazuri tu tukimuamini yeye tu!"