Friday, December 23, 2011

MWISHO WA DUNIA SASA?


Huko Namibia kidude kimedondokea ardhini na hamna anaejuwa ni kitu gani; na taifa sasa limeomba msaada ng'ambo ili kupata maelezo kwamba ni kitu gani.


Aina yake lakini ni chuma. Urefu kama mita moja.


Hata hivyo hamna aliejitokeza hadi kwa wakati wa uchapishaji wetu ili kukiri yeye ndie mwenye chombo (yaani mtu au taasisi yoyote ile kutoka katika mataifa yenye kurusha vyombo angani kama satelaiti).



Wacha nilete utund wangu kidogo: Na kama kidude kingemtoa mtu roho je...? Nani angemlipa fidia?


Tusubiri basi kusikiliza haya mambo yanaelekea wapi.


Binafsi nimeshangazwa pia na maumbile yake... kama nini vile... basi tena! Ngoja nisimame hapo hapo!



6kg metallic ball drops from the sky in Namibia - Times LIVE:

'via Blog this'

2 comments:

  1. Duh! Mungu tusaidie usiwe mwisho wa Dunia hapa inabidi tuwe na imani

    ReplyDelete
  2. Kwakeli da'Yasinta,mbona mambo ya ajabu ajabu naya kutisha?Mungu tubariki.

    ReplyDelete