Credit for the following story (rendered by yours truly in Kiswahili) goes to Mrs Simangele Matsebula of Barberton/Emjindini (wherever she got it from to ruin my evening with another post for this blog when I was all set to finalize my polishing-up process in Pitman Shorthand instead)
DOMO CHAFU NA MWENYEWE
(UDLAMINI ONGAHLONIPHIYO)
Huu ni mwaka 1956 Afrika Kusini Johannesburg, kwenye migodi. Mzee Dlamini kutoka Swaziland naye ni mmoja katika walala hoi kutoka KwaZulu Natal, Lesotho, Swaziland na nchi mbalimbali kutafuta riziki hapa kwa kuchimba dhahabu. Mzee Dlamini alikuwa ni yeye tu mwenye uwezo wa kusoma; na wengine wakaanza kumtegemea yeye ili awasomee barua zao kutoka nyumbani kotekote. Hasa Wazulu walimpenda sana Dlamini kwani aliongea Kiswazi sawasawa kabisa kama anavyoongea Kizulu.
Hata hivyo, Mzee Dlamini alikuwa nayo kasoro kubwa. Ulimi wake ulikuwa mbaya sana; yaani baada ya kusoma barua ya mtu, alikuwa hana uwezo wa kupunguza makali ya ujumbe na alikuwa anamwambia mtu kinaganaga. Mfano: “Fulani, Mke wako anaomba talaka” au, “Fulani, mtoto wako amekufa”.
Kutokana na hayo, siku moja wafanyakazi wakamweka kikao; na kumwambia awe muungwana kidogo anapotoa ujumbe. Naye akakubali atajitahidi.
Ndipo ikaja barua moja kumweleza Mzee Nxumalo kwamba bibi-mtu (mzaa-mama) ameifariki dunia. Naye Dlamini akaitisha kilekile kikao kukieleza tukio au ujumbe wa barua hiyo. Pia aliwataka wamuone kwamba ameshajirekebisha na sasa yeye ni mwangalifu wa jinsi anavyotoa ujumbe wa kusikitisha.
Kilipotimia kikao, akawaambia: “Jamaani, yee! Ninao ujumbe kuhusu mmoja kati yenu hapa; lakini na ogopa kuyasema ya mule kinaganaga. Kwa hiyo nitaomba kila mmoja wenu mwenye kuwa na bibi hai asimame... bibi mzaa-mama lakini... SIMAMENI!”
Wahusika ndiyo walisimama! Naye Mzee Nxumalo aliekuwa anampenda sana bibi yake alisimama.
Ndipo Dlamini akasema: “Kaa chini, wewe Nxumalo! Nakusihi sana, kaa chini kabisa!”
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Mwisho wa stori. Sijui kama umeifurahia kama inavyofurahisha mtu unapoisoma kwa lugha ya Kizulu, moja ya Vingoni vya Afrika Kusini. Kumbuka, unapoongelea juu ya Kingoni/IsiNguni cha hapa Afrika Kusini ni lugha nyingi vinavyozungumzwa na Wangoni/AbeNguni hapa, nao wakiwa Wazulu/AmaZulu, Waswazi/Emaswati, Waxhosa/AmaXhosa, Wandebele/Amandebele
Kumbuka pia: Ukijifunza lugha moja katika ya hizo zilizotajwa juu,basi umejifunza yote. Stori ya Mzee Dlamini iko katika lugha ya Kizulu. Inahusu maisha ya Afrika Kusini kwenye migodi. Kama mnavyojuwa, wengi sana Waafrika kutoka Tanzania, Malawi, Zambia, Msumbiji, Swaziland, Lesotho, Namibia etc walimiminika Afrika Kusini karne iliepita kufanya kazi za migodi, yaani kuchimba dhahabu. Wengi wao walikuwa hawakusoma kabisa. Vingoni vya Afrika Kusini na Kiswahili vimekaribiana cha kushangaza sana; na mwenye lugha ya Kiswahili anapovisoma, atagundua maneno mengi sana sawasawa naKiswahili. Lakini mtihani mkubwa kuliko yote ni kule kuweza KIVISOMA.
Leo naonyesha baadhi ya herufi za kuzingatiwa ukiwa unajifunza Vingoni vyenyewe kwa msimamo wako waKiswahili.
HL= NA ULIMI (tongue)WAKO, gusa meno yako makubwa (MOLARS AND PREMOLARS) na puliza BILA KUTOA SAUTI!! Ukitoa sauti itakuwa DL!
C=weka mate kidogo mwanzoni wa ulimi wako(THE TIP OF YOUR TONGUE), gusa paa ya mdomo (THE ROOF OF THE MOUTH/ THE PALATE) na ulimi huo sehemu yenye mate na vuta hewa kutoka upande wa nje wa mdomo ukivutia upande wa ndani LAKINI USITHUBUTU KUHEMA AU KUVUTA PUMZI (IN OTHER WORDS, YOUR WINDPIPE SHOULD NOT BE INVOLVED IN THE SUCKING-IN PROCESS!) NA HUO NDIO MSINGI WA-clicks c,x,q ZOTE KATIKA VINGONI).
X= Ni nduguye “C”, na ni mlio wa chura! Hata chura mwenyewe Wazulu wamuita ‘ixoxo’! Mwanzo wa ulimi wako (YOUR TIP OF THE TONGUE) unagusa nao paa ya mdomo lakini nyuma iwezekanavyo, halafu vuta hewa LAKINI, TAFADHALI, MARA YA PILI, USIHEME! NA PILI, UNAPOVUTA HEWA HIYO HAKIKISHA INAINGIA CHINI YA ULIMI WALA SIO JUU KAMA ULIVYOFANYA KWA MATAMSHI YA “C” HAPO JUU)
Kh= Soma vile kama hamna ile “h”, NA TAFADHALI, USISOME KAMA UNAVYOSOMA KISWAHILLI MANENO KAMA “SHEIKH” “YAKHE” “KHARTOUM”!
Th = NAYO SOMA VILE KAMA HAMNA ILE ‘H’!
Ph= SOMA VILE KAMA HAMNA ILE “H”
========================================
Haya basi, kwa lugha ya Kizulu (pamoja na tafsiri yangu uchwara kiasi hata kutafsiri pia majina ya watu), stori yako hii hapa chini. Herufi zile zenye mataamshi magumu kidogo nimezipigia mstari kwa manufaa yako msomaji, lakini hadithi ukiiisoma kwa kurudia na kwa kupaza sauti utazowea siku moja kutamka Kingoni cha Bondeni huku. (Mimi nitapata furaha siku moja ukinitumia barua/EMAIL na kuniambia wewe Fulani bin Fulani uko tayari kunipigia simu unisomee hadithi hiyo... nitakupa nambari yangu ya simu ukiwa tayari ili nipate uhondo wa matamshi yako!)
UDLAMINI ONGAHLONIPHIYO
uDlamini kwakunguye yedwa okwazi ukufunda eMayini bonke abanye befundelwa nguye izincwadi zabo, into eyayibakhathaza abantu ukuthi wayehlambalaza nje, engakwazi ukubeka kahle indaba Isibonelo: wayevele athi "Ndlovu ufile umama wakho hamb'ugoduke.” Wabizelwa umhlangano uDlamini bamcela ahlele kahle amagama akhe uma edlulisa umbiko, walalela uDlamini. Kwafika incwadi ebika ukuthi akasekho ugogo kaNxumalo ...ngokuzithoba okukhulu uDlamini wababiza bonke, wathi mabaphakame bonke abanogogo. Baphakama abantu. Wayesethi -"Hlala phansi wena Nxumalo. Awusenaye ugogo!"
MALAMCHANA ASIEWAHESHIMU WENGINE
Malamchana ilikuwa-yeye peke-yake anaejuwa kusoma Kwenye-migodi wote wengine wakiwa-wanasomewa ni-yeye barua zao, kitu kiliowakera watu ni-kwamba anakashifu tu, hakuwa-na-uwezo “kuweka”/kueleza vizuri habari Mfano: “angalijitokeza”/angalikurupuka nakusema "Mzee-'Tembo', amekufa mama yako nenda’uondoke”. Walimuitia kikao Malamchana wakamuomba “alolonge”/aeleze vizuri maneno yake ikiwa anapitisha ujumbe, alisikilliza Malamchana. Ilifika barua yenye-kutaarifu kwamba “hayupo-tena”/amefariki bibi yaNxumalo ...kwa-unyenyekevu mkubwa Malamchana aliwaita wote, alisema wasimame wote wenye-bibi. Walisimama watu. Ndipo-alisema -"Kaa chini wewe Nxumalo. Huna-tena bibi!"
Kwastori hii namshukuru dada mmoja wa huko Barberton/Emjindini, Bi Simangele Matsebula
Ngalenganekwane lena ngibonga omunye udade wa le eBarberton/Emjindini, uNkosikazi Simangele Matsebula.
Kusudi upate mataamshi zaidi ya Kingoni cha Bondeni, bonyeza hapa.
No comments:
Post a Comment