Saturday, November 12, 2011

MAOMBOLEZO YA KUUWAWA KWA MUAMMAR GADDAFI YAMTAKA RAISI A.KUSINI AJIUZULU

South African Julius Malema:
A Wounded Tiger Going For Scalps






JOHANNESRBUG, BENONI.


Afrika Kusini hapa mwakani (2012), wakati kama huu na mwezi kama huu, jinsi anavyohisiwa kulenga Raisi wa Nchi hii, lazima awe tayari keshapata uhakika ataliongoza taifa miaka mitano zaidi.  Lahasha, viongozi wa Umoja Wa Vijana wa Chama Tawala ANC, kinaganaga wamemuambia leo yeye wanayemlaumu kwa kifo chake Kiongozi wa Libya, Marehemu Kanali Muammar Gaddafi: [‘Ondoka madarakani, kwani hujui unalolifanyia Bara kama kiongozi Wa Afrika tena Who killed Gaddafi while we still loved him?’]



 “[Toka zako, na kama ikiwezekana, toka kabla ya Kongamano la Chama ANC mjini Mangaung mwaka 2012 Mwezi Disemba, wanamwambia Mzee maskini aliejipatia sifa mbaya ya kukimbiza watoto wadogodogo kama vijana haohao wanaompinga leo. “Kwani wewe ndiye uliesababisha Wazungu na majeshi yao ya NATO wamfanyie unyama Mzalendo Gaddafi wa Libya kwa kura yako uliyewapa hao Wazungu na na serekali zao za ukoloni-mamboleo huko Umoja Wa Mataifa]”.




Leo, ikiwa Jumamosi, viongozi wote wa Vijana hao (ANC Youth League) walikusanyika mjini Benoni (karibu na Johannesburg) na wametoa kiapo [“Mzee tunakuambia unaondoka tu wewe upenda-usipopenda; na sisi tu’amtaka sasa naibu wako atufanyie leo dua kwa Mwenyezi-Mungu ili tukung’oe madarakani sisi vijana wa Nchi!  Yeye Naibu ndie atashika hayo madaraka, lakini naye achunge sana kwani sisi hatumpendelei kutokana na kidevu chake kama cha mbuzi (GOATEE) bali tutamtaka ataifishe migodi yote ya Afrika Kusini pamoja na kutupatia shamba za kulima bure kwa Wazungu waliyewanyang’anya mababu zetu shamba hizo karne zilizopita”].


Msomaji wa blogu yangu hii, kuwuelewa mzozo huu lazima nikuhabarishe kwamba, hadi sasa hivi, duniani kotekote kulipojaa dhahabu, Afrika Kusini ni moja ya nchi tatu zenye machimbo ya dhahabu mengi kuliko nchi zote zingine.

Elewa kwamba migodi huku inatoa pia madini ya Uranium inayosaidia sana matibabu hospitalini, nguvu za kuendesha vyombo vyaangani, pia na kutengeneza silaha za kuteketeza kama Nuclear.


Afrika Kusini imejaa tele madini mengine ya thamani kubwa hata kuliko dhahabu. 

Nchi hii pia ni kiongozi kipaumbele kuliko nchi zote duniani katika kutoa madini aina ya Platinum ambayo nayo ni madini ya thamani kuliko dhahabu.



Pamoja na utajiri wote wa nchi hii (unaowafanya matajiri wa Afrika Kusini kuwa ni wajuu zaidi kuliko wengine ulimwenguni kote ukilinganisha na kiwango cha shida ya walala-hoi), umaskini Afrika Kusini hasa kwa Waswahili wasikitisha mno.  Na jiji likikushinda, Mswahili wewe maskini huna uwezo wakwenda kulima “vijijini” kwani nchi yote yenye rutuba iko mikononi ya wachache wale wale waliekuwa wananufaika enzi za Apartheid.

Kwa hiyo watu wamezidi kumiminika mijini ambapo watoto wao hawaendi ya kutosha shule kutokana na ada juu kwa shule au njaa; na matokeo yake inakuwa rahisi sana kueneza na kuhalilisha ujinga zaidi wa kisiasa unaohalalishwa mara hadi mara na viongozi katika Chama wanao amini eti

[“Elimu ya bure haiwezekani”]

[“Unaweza ukajikinga na ukimwi kwa kuoga tu baada ya kufanya mapenzi, au ukishaambukizwa wewe kula tu vitunguu vingi”]

 [“Vibaya kuwapa Waswahili bure baadhi ya mashamba ya Wazungu bila kuwalipa hao mabilioni yatakayeitia serikali umaskini wa bure kwa Waswahi wengi wavivu kulima”]

[“Watanzinia, Wazimbabwe, Wazambia, Wanigeria na Waafrika wengine nchini Afrika Kusini wanawaibia wenyeji ajira na kusababisha umaskini nchini”]

[“Kabila la Kingoni anakotokea raisi wakwanza nchini ndilo kabila lenye akili kuliko makabila mengine nchini na wengine, isipokuwa Wazungu tu, ni wajinga tu hata wakisoma namna gani”]

 [“Kutaifishwa kwa migodi Afrika Kusini kutasababisha Wazungu wa Ulaya na Amerika kuitia Afrika Kusini vikwazo vya uchumi kama Zimbabwe”]



Maoni-potofu yote kama hayo ya juu (baadhi yake yakitamkwa na zaidi ya mmoja katika maraisi wa chama tawala)  [yanalaaniwa daima hadi leo] na ANC Youth League (Umoja WaVijana) ["kama ndoto tu ya Wazee wanaotumia sifa nzuri za chama ANC ili kujinufaisha wenyewe mbele tu kwao anasa na wizi wa hela za umma wakati umma bado unateseka na ufukara wa makusudi, ubaguzi warangi yaMzungu, ukabila wa viongozi wanaotawala na chuki dhidhi ya Waafrika wenzao"]. Ndio maana wanamtaka Mzee wa Chama tawala na Katibu Mkuu  wake, [“wapotelee mbali hata kama uwezo wakuwapoteza mbali unahitaji wao wakiwa viongozi wa Vijana wapewe kifo au kusimashwa uongozi kama vile alivyosimamishwa Kiongozi wao Julius Malema punde Alhamisi 10 November 2011”]

Moja ya marufuku kubwa nchini A. Kusini ni utani, na katika hoja za msukosuko katika chama tawala nahisi nitakuwa wakwanza kusema huenda pia sababu ya kusababisha makofi wanaotiana hawa wakubwa kwa wadogo wa chama. Ni ukabila. Kitu kama zaidi ya miaka 50 iliepita sasa hajatokea hata mara moja Msouth Afrika kuongoza chama hiki asietoka katika ka Wangoni/Nguni, kwani wote ni Wangoni tu kutoka kwa huyo anayetawala sasa, wende kwa Mbeki, kwa Mandela, kwa Tambo, kwa Luthuli aliyeanza kukitawala chama mwaka 1952.

Yaani kwa miaka 60 kwa mia ya maisha ya chama miaka mfururizo hadi leo wanatawala watani wawili tu, na hamna hata mmoja alieruhusika (na tumia neno kwa uangalifu) kukiongoza hata siku moja chama hiki akiwa anatoka kabila la Waswazi, wala Wapedi (anakotokea Julius Malema karibu na Zimbabwe), Wala Wasotho, Wala Machotara, Wala WaTonga/Shangaan, Wala Wavenda (alikotokea Cyril Ramaphosa), na kadhalika.

Mwandishi nashindwa kuamni makabila yote hayo ni wavivu wafikra za uongozi au waoga dhidhi ya Wakoloni-Mamboleo na Apartheid Barani, miaka yote hiyo.  Maoni yangu yatastiri dhidhi ya mashambulizi yoyote yale ukizingatia kwamba viongozi-majeruhi ya siasa yaMzee leo 2011 (wavulana Julius Malema, Floyd Shivhambu, na msichana Kenetswe Mosenogi wote wakiwa vijana wa ANC Youth League waliopewa adhabu kali za kipuuzi lakini ikiwa ni kutokana na kuitikisa siasa ya nchi nzima karibu miaka mitano sasa), hamna hata mmoja mwenye kabila la Wangoni.

Maana yake ni kwamba: binadamu sote ni sawa na hamna kabila janja kuliko mengine.  Sasa iweje chama kitawaliwe na mtu mmoja miaka na ndugu yake alazimishe kukiongoza chama hicho kinapoanzisha karni ya pili katika maisha yake mwakani?  Kama miaka 60 iliepita iliongozwa na ukabila wa kisirisiri, nani ataminga Phiri leo nikihisi moja ya vipengele vikubwa katika huu mzozo ni uchovu mtupu katika makabila ya Afrika Kusini na kuongozwa na watu tu  wanaotoka Jimbo majimbo mawili tu katika tisa nchini kote miaka yote?


Mwandishi hapa ningependa sana pia binafsi kumtetea Raisi wa Sasa Afrika Kusini, akiwa Mzulu (na moja katika makabila ya Wangoni) wakwanza kukitawala chama kwa miaka 45 mfururizo wa utawala wa kabila lake Bw Mandela.  


Kifupi, yote matatizo yanayokiumbisha chama cha ANC hayakuanzishwa naye.  Hata wito matumizi ya vitunguu badala ya madawa ya ukimwi ulianza na Raisi Thabo Mbeki, mmoja katika watu inaosemekana ni msomi sana kutoka  Kabila Hilo-Hilo Miaka Arobaini Na Tano.

Kama ni hiyvo, sasa kosa lake Raisi Nxamalala (jinsi linavyotamkwa jina lake hapa kwa heshima) ni nini?  

Ingewezekanaje ugonjwa uliyeanzishwa na Bw. Mandela miaka 17 (au miaka 33 kabla ya uhuru) iliepita kupata tiiba chini ya miaka miwili au mitatu tu ya uongozi wake Nxamalala?

Wanamuonea bure Mzulu wa watu kwa kusadiki eti kwasababu yeye aliacha shule darasa la nne kwa hiyo yeye ni mjinga!  Au wanataka naye sasa apate kusafirishwa duniani bure kama vile walivyomfanya Albert Luthuli (Mzulu wa mwisho kukitawala chama na kung'olewa madarakani 1967 kwa kukaabwa na kisha kutupiliwa maiti yake juu ya reli ili kusingizia aligongwa na treni mwaka huo wa 1967 uliyeanzisha huo utawala wa kabila moja tu hadi kuingia madarakani kwake Nxamalala?


Naona wengi zaidi ya hawa watoto rafiki zake Julius Malema waliekuwa na mkutano wao wenye kejeli huko Benoni leo na kumsifu jambazi marehemu” Gaddafi aliekuwa anakinyima chama cha ANC mapesa ya kupigania uhuru” (kama alivyonukuliwa Raisi Mstaafu Thabo Mbeki mwanzoni wa wiki hii akisema) wataendelea tu kupata adhabu kali sana kutoka katika Chama-Mzazi (African National Congress) kinachotimiiza miaka 100 mnamo tarehe 8 Januari 2012!

Kiongozi wa vijana mwenyewe huyo Julius Malema siyo tu kama amesimamishwa kazi ya chama miaka mitano, ripoti zinamimika kila sekundi kwamba vyombo vya dola vitamtia mbaroni kwa kupokea hela za rushwa kutoka kwa wanabiashara kadhaa nchini.  Lakini haki niandike pia kwamba yeye tayari kujitetea hata kabla ya kukamatwa wala kusomewa mashtaka, na anasema: [“Nitapewa na nipokee rushwa kivipi ikiwa kijana mie sina kazi hata moja serikalini? 

Anaongeza kishupavu kama vijana wenzake Shadrack Meshack na Abednego wa Maandishi Matakatifu:[Nitieni mbaroni tu na nipeni kifungo cha kutumikia jela kwa kutetea nchi yangu tu wala isiwe kisingizio za kula rushwa.  Na huko jela kama mukithubutu kunifungia visingizio kama hizo, Mungu wangu atanipatia kazi takatifu ya kuwaelimisha siasa wafungwa wenzangu, poteleeni mbali na mtafute pingu za kunifunga sasa hivi kama mnaweza!”]

 Kwa kweli, vita vya wenyewe kwa wenyewe Afrika Kusini lazima maiti yatatokea tu, nasi waandishi hatupo salama kabisa...kesho keshokutwa mnaona blogu kimya mjue mtu amekwenda tu na maji ya haki na fursa zilizopotezwa mnamo mwaka 1994 kutokana na makubaliano ya uhuru wa bendera tu kwa Mswahili ikiwa bado uchumi na mali uko palepale ulipokuwepo kabla ya hapo.







Motlanthe pray for us – ANCYL, November 12 2011 at 04:41pm

African National Congress Youth League President Julius Malema led the League's National Executive Committee (NEC) meeting in Benoni on Saturday.
Malema - who has been suspended for five years after the ANC's National Disciplinary Committee found him guilty of bringing the party into disrepute - danced and sang alongside his fellow comrades.

“No matter how difficult, we are going to Mangaung, even when they suspend us,” NEC members sang in isiZulu.
The closed meeting was believed to have been called to discuss the League's reaction to the suspension of Malema.  During a brief photo opportunity members of the NEC outlined their intentions at the 2012 Manguang conference in song.

“2012 siVota Mbalula, siVota Kgalema” they sang.
The League wants Sports Minister Fikile Mbalula to replace Gwede Mantashe as the African National Congress's secretary general. They also want deputy president Kgalema Mothanthe to be elected president of the ANC.

Mbalula is a former president of the ANC Youth League.
The ANC holds its elective conference in Mangaung in the Free State in 2012.

“Mantashe wa sokodisa...Motlanthe o re rapedise re masokolara,” which loosely translates to 'Mantashe is annoying...Motlanthe pray for us we are suffering,' they sang while photographers took pictures

The tempo increased when they sang a song about nationalisation of mines: “Motlanthe go tlo ba monate ga re nationalisa di mine tsa SA (Motlanthe it will be nice when we nationalise all mines in South Africa).”

They concluded by singing a song in respect of slain Libya ruler Muammar Gaddafi.

“Who killed Gaddafi while we still loved him” they sang in IsiZulu.

3 comments: