1.
Nimekwishajifunza tabia labda mbaya sijui au
nzuri ya kutumia maneno kabla ya kuthibitisha uwerevu wangu juu yake.
2.
Kwa mfano: nini
“kutambika”?
3.
Kichwa chake cha Kiswahili-uchwara kimeniambia
ni ile namna Mswahili (yaani “African”) anavyojizatiti kuungana au kupata
maongezi au hata mawasiliano na Muumba wake kwa kuwapitia mababu na mabibi
waliotangulia…..
4.
Hakika nitarekebisha makosa katika posta/post
hii kama hapo baadaye najikuta sikuelewa kabisa maana ya KUTAMBIKA
TAMBIKO. Lakini nimeandika hivyohivyo
kwasababu nimejifunza kitu kimoja maishani: ukitaka kuelekewa unamaana gani
ANDIKA TU KAMA ROHO INAVYOKUTUMA NA REKEBISHA VINGINE HAPO BAADAYE LA SIVYO
UTAITSHIA HUTAANDIKA LOLOTE KWA OGA WAKUKOSOLEWA NA MABINGWA BILA MAPROFESA YA
LUGHA AU UJUZI NA TAALUMA FULANI AMBAOWEWE KAMA MWANDISHI HUNAYO. Kwa hiyo: Potelea mbali ukiwa mwandishi
mwenye kutaka uhakika juu ya hisia zako!
5.
Turudie basi katika namna ya kuhusiana na Mungu
wangu au wako.
6.
Kila dini (na dini ni nyingi hapa Afrika
zinakaribia kunichefua mimi binafsi kwani uwingi wake siwuelewi ikiwa Mungu ni mmoja)…lakini kila dini itakwambia jinsi gani ya kujijumiisha na Muumba. Tatizo ni kwamba kila dini hiyo imeandikwa
aidha na Wazingu au Waarabu au watu wa Asia NA WANAMWAMBIA MWAAFRIKA HUYOHUYO
MMOJA.
7.
Mimi binafsi sikatai dini yoyote; ila
nimejifunza kwamba dini yoyote ile haina maandishi yoyote yenye kukana au
kupindua mila na desturi za Kiswahili au Uafrika na jinsi sisi Waafriak an
Wakongwe wa Ubinadamu Wopte tulivyokuwa tunawasiliana na Mungu hata kabla ya
kuzaliwa kwa Kristu, Buddha au Muhammad.
Na kwahiyo l eo ningependa kujumuika nawe kama msomaji wa blogu yangu
jinsi nilivyoelezwa Mswahili (African) wakwanza (hata kabla ya kuzaliwa kwa
Mzungu, Mwarabu, au Mchina) alivyokuwa anawasiliana na Mungu wake.
8.
Nitakachokieleza siyo siri yangu wala maandishi
matakatifu, bali ni kile nilichoelezwa na wazee Afrika Kusini hapa; na naomba
mwenye ujuzi zaidi yangu aongeze kwa maoni yake udhaifu au nyongeza vikiwa
vinafaa katika maandishi yangu. Kwa yote
lakini mimi ni mwenye imani ya kwamba Mswahili (African) ameshindwa kuwa mtu
katika watu wa dunia kutokana na usiri wake katika mambo yenye kumnufaisha yeye
kama dini yake ya kiasili. Mswahili pia
anaaibu sana kujitangaza na kujitembeza, ikiwa ukweli ni kwamba kama lipo taifa
lenye sababu la kujigamba kwa chochote kkile, HAMNA LINALOMPITA AU KUMSHINDA
MSWAHILI, KWANI SISI WASWAHILI NI BABU AU BINI ZA BINADAMU WOTE DUNIANI.
9.
Kifupi sisemi acha uKrestu au uIslam wako; bali
nasema, bali nasema: kusudi bara letu Afrika liende mbele, tafakari vile jinsi
Waswahili (Africans) wengi wanavyoendesha maisha yao ya kiroho (spiritual lives).
Kwahiyo nakupa katika maandishi ya fuatavyo jinsi nilivyo elimishwa mwaka huu
2013 namna ya kupata mafanikio maishani yako, au kushinda mitihani yote.
10.
Kwanza lazima ujuwe nani ukoo wa baba yako mzazi
au pamoja na baba yako mlezi.
Hivyohivyo kwa upande wa akinamama.
11.
Jaribu kujifunza kuhusu mambo hayo kwa kuuliza
vitu kama kabila lako na historia kifupi ya na kirefu ya familia yako mazuri na
mabaya.
12.
Tafakari au elewa wale watu wa zamani wenye ukoo
wako walikuwa wanakula chakula gani… pata ukweli hasaa juu ya huyo babu au bibi
unaependa kumsihi akusaidie katika matatizo yako
13.
Ukishapata walikuwa wanakula chakula gani,
tafuta unga kidogo sana ili kuwapa WALE.
14.
Labda pia walikuwa wanywaji… sasa pombe gani
ilikuwa…FANYA UTAFITI KWA KUWAULIZA WAZEE! (mfano baba yangu mzazi alikuwa
mnywaji wa Bols Brandy, na Richelieu na kama namwaza yeye ataweza kuliko
wengine kunielewa sioni sababu yakutonunua
kiwango kidogo cha BRANDY yake kumfurahisha)
15.
Kingini cha kwelewa ni kwamba JE WALIVUTA NINI?
Afrika Kusini tunaimani kwamba wote wazee wetu wa kale hawakuvuta chochote bali
walikuwa watumiaji wa ugoro…. Hapo ni
kazi kwako mwenyewe….
16.
Kwa hiyo ugoro kidogo karibu utakamilisha labda
maandalizi ya maombi yako kwa Mungu na kwa wale waliekuwa karibu naMungu wakiwa
ndugu zako.
17.
Cha mwisho kabisa labda ni maji: binadamu yeyote
aliyewahi kuishi duniani hakuweza BILA MAJI, na kwa hiyo KWANINI UWANYIME MAJI
WALE WALIEZOWEA MAJI.
18.
Baada ya kuandaa chote utakayewapa hao Wazee wa
kale, kunavipengele kadha wa kadhaa lazima uelewe kabla ya kuwapa
wajiburudhishe kwa wakati watakopofikiria jinsi ya kukusaidia katika matatizo
yako (SI UNAKUMBUKA YOTE HAYA NI JINSI YA KUJITOA KATIKA MATATIZO FULANI…KESI
ZISIYO KUWA NA MWISHO…KUKOSA MPENZI…KUSHINDWA BIASHARA… AU HATA KUSHINDWA KURA
KWA WANASIASA…??)
19.
Kama unaishi nyumbani kwa mzazi wako sawa kabisa
kwani yote utafanya kama kawaida. Lakini
kama umepanga unanisoma blogu yangu uko hotelini pahala Johannesburg, Dar es-Salaam, Kenya au hata
Tokyo LAZIMA UTOKE KWANZA WENDE PORINI. Ndipo huko utakapowataja wote mababu na
mabibi zangu HALAFU KUWAMBIA “KWA SASA HIVI JAMAANI NIKO HAPA NEW YORK,
LONDON,AU JOHANNESBURG NIMEPANGA HOTELINI NA NAOMBA MUNIFWATE NIKAWAONYESHENI
NINAPO ISHI”
20.
Hapo ulipo ndipo utakapowapea vyakula na vinywaji
vyao pia na ugoro au uvutaji wao kama walivuta hiyo bangi, tumbako au chochote
kila kutokana na utafiti wakowa ukoo wa zamani. (WENGINE LAKINI HAWAONI KOSA LA
KUWAPIA VYAYO HUKOHUKO MISITUNI KAMA WEWE HAUPO NYUMBANI)
21.
Sasa Bibi wa miaka 70 aliyenifunza mwaka huu
yote haya alijumuuisha hata mambo ya kutapika name kama mwanafunzi wake nifuata
na kufanya inavyostahili kwani alisema ni muhimu ili usiwe na nuksi (nilikuwa
naanda kwenda kortini). Binafsi lakini nafikiri mambo ya kujifanya utapike ni ujinga
mtupu, lakini labda mmoja wa wasomaji
ataniona kosa kama sielezi namna yake, nayo ni hii:
22.
Robo kikombe ya ‘diwani’ (kama ndio neno sahihi
la ‘VINEGAR’) na robo ya kijiko chumvi katika maji vuguvugu kitu kama lita
mbili…kunywa asubuhi AU kabla ya kuongea
na Wazee wako au bada…na ingiza au mkono au chocho chenye kusabisha matapiko ya
maji hayo. Hapo ndipo umejifanya ‘msafi’ kwa watu wadunia utakavyokabiliana
nayo kwa siku hiyo.
23.
Ningependa kumalizia hapa kwa leo,bila kusau
maelezo ya fwatao. Posti hii nimefanya kutokana na kwamba sisi WaSwahili ni
wasiri sana kuhusu mila na desturi zetu name nafikiri huo ndio ujinga wa
kupindukia kwani atajuwaje mtoto aliyekuwa Chuo Kikuu kuhusu mambo yetu kama
hatuandiki? Vilevile usiri wetu huo pia
umesababisha matapeli wengi sana kutuibia hela zetu huku wakidai
wanatuunganisha na Wazee wetu.
24.
UKWELI NI KWAMBA HUITAJI MGANGA YOYOTE ILI
KUTATUA MATATIZO YAKO NA MUNGU AU WAZEEWALIEKUFA! UNAHITAJI TU KUWAELEWAWAO
WALIKUWA AKINA-NANI NA WALIPENDELEA VYAKULA GANI NA “WAPE BASI VIDONGE VYAO ILI
NAO WAKUPE SULUHISHO KATIKA TATIZO LAKO”
25.
P.S.
Hakikisha kwamba unapoongea nao hao wakubwa MASHARIKI INAKAA KUSHOTO KWAKO!!! (yaani
unaangalia kusini mwa ardhi alipoanzia maisha yake Binadamu yote duniani)
Tambiko ni tambiko hata akiwa anamtambika Yesu, Muhammad, Buddha au Babu au Bibi yake Mungu hata ubaguzi juu ya kumpa majibu kutokana na maombi yake pia na ukweli na uaminifu wa roho yake |
No comments:
Post a Comment